Wachezaji wa Stars wa mwaka 1980 wapatiwa majina ya Mitaa

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars )

Kata ya Kigoma imetoa mitaa 25 kwaajili ya kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kilichoshiriki michuano ya AFCON mwaka 1980.
Kufuatia vikao vilivyofanyika katika kata hiyo vya kupanga majina ya mitaa imeamua kutoa mitaa hiyo kwa wachezaji na makocha wote waliyoshiriki michuano hiyo kwenye eneo la Mji Mwema.
Kata hiyo pia imetoa jina la Prof. Abdulrahman Mohamed Babu kwa mchango wake Afrika na ukombozi wa Afrika.
Kikosi cha Taifa Stars cha mwaka 1980 hiki hapa
Athumani Mambosasa
Juma Pondamali
Taso Mutebezi
Jelah Mtagwa
Leodgar Tenga
Mohamed Kajole
Husein Ngulungu
Mtemi Ramadhan
Juma Mkambi
Omari Hussein
Mohamed Masewa
Thuweni Ally
Peter Tino
Ahmed Thabit
Charles Boniface
Salim Amiri
Adolf Richard
Zamoyoni Mogela
Martin Kikwa
George Kulagwa
Uzinduzi wa mitaa hiyo ya mashujaa unatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi ya kwanza ya mwezi wa tisa ambapo kutachezwa mechi kati ya timu ya Manispaa ya Lake Tanganyika SC na timu ya Bukavu Dawa ya DRC.
Post a Comment
Powered by Blogger.