Rais Magufuli amteua Waziri Kindamba kuwa ofisa mtendaji mkuu wa TTCL

Rais John Magufuli amemteua Waziri Kindamba kuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).
Taarifa iliyotolewa leo (Julai 6) na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imesema uteuzi huo umeanza Julai 4.
Kabla ya uteuzi huo, Kindamba alikuwa akikaimu nafasi hiyo.
Kindamba aliteuliwa na Rais Magufuli kukaimu nafasi hiyo Septemba 23 mwaka jana.
Baada ya uteuzi wake, aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura ilielezwa atapangiwa kazi nyingine.
Taarifa ya Ikulu iliyotolewa wakati huo ilieleza uteuzi wa Kindamba ulitokana na Serikali kununua hisa zote za Bharti Airtel aliyekuwa mbia mwenza wa TTCL na hivyo Serikali kumiliki hisa za kampuni hiyo kwa asilimia 100.
Post a Comment
Powered by Blogger.