PICHA: YALIYOJIRI KWENYE MECHI YA EVERTON NA GOR MAHIA

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MSHAMBUALIAJI hatari wa Everton, Wayne Rooney, ameonyesha kuwa yeye ni gwiji wa kupachika mabao baada ya kufunga goli umbali wa mita 25, kutoka lango la Gor Mahia ya Kenya katika pambano la soka la kirafiki lililoandaliwa na wadhamini wa timu hiyo, SportPesa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo Julai 13, 2017.
Rooney amabye alicheza kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza, alikuwa akichungwa na walinzi kadhaa wa Gor Mahia katika kipindi hicho cha mzhezo, lakini kutokana na umahiri wake, alifumua shuti la kushtukiza na kujaa wavuni kuandika bao la kuongoza ambalo halikudumu kwa muda mrefu kabla ya Gor Mahia kusawazisha bao hilo. Everton walipachika bao la pili katika kipindi cha pili na hadi mpira unamalizika Everton iliibuka mshindi wa mabao 2-1. Katika tukio lingine shabiki wa soka alichomoka kutoka kona ya Mashariki mwa uwanza wa Taifa na, "kuzama" uwanjani moja kwa moja na kumkumbatia Wayne Rooney ambaye kabla ya kurejea Everton alikuwa akiichezea Manchester United. Polisi walijaribu bila mafanikio kumfukuza kijana huyo ili asimfikie nyota huyom wa ligi kuu ya Uingereza. Kijana huyo aliyevaa jezi ya Manchester United, alifanikiwa kumfikia Rooney na kumkumbatia kabla ya polisi kumtia mbaroni na kutoka nae nje ya uwanja. Hata hivyo ilitangazwa uwanjani hapo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. aliamuru kijana huyo aachiliwe huru kutokana na kitendo chake.
Gor Mahia imefanikiwa kucheza na Everton baada ya kunyakua kombe la SportPesa super cup 2017. timu zote hizo zinadhaminiwa na SportPesa.
Pichani Rooney akijaribu kumtoka mlinzi wa Gor Mahia. Rooney akikumbatiwa na kijana huyo aliyejitoa "muhanga" kuingia uwanjani wakati pambano hilo likiendelea.
 Rooney akipomgezana na wachezaji wenzake baada ya kupachika bao hilo.
  Rooney akipomgezana na wachezaji wenzake baada ya kupachika bao hilo.


Post a Comment
Powered by Blogger.