Picha: Mazishi ya Bradley Lowery yafanyika nchini Uingereza

 Mtoto Bradley Lowery ambaye alifariki wiki iliyopita baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kansa kwa muda mrefu hii leo amezikwa huko nchini Uingereza.

Katika ibada maalum ambayo ilifanyika katika kanisa la St Joseph ilihudhuliwa na watu wengi waliovaa jezi zake huku rafiki yake kipenzi Jermain Defoe akionekana kutokwa na machozi.

Barabara za kuelekea kanisani zilipambwa na jezi zenye jina lake na maputo yaliyokuwa na rangi ya Everton huku mashabiki wa timu nyingi barani Ulaya walionekana.
 Lowery ambaye alikuwa ni shabiki namba moja wa Sunderland alifariki kufuatia kusumbuliwa kwa muda mrefu na maradhi ya saratani yaliyochukua maisha yake katika umri wa miaka sita tu.
 Nyota wa timu ya Taifa ya Uingereza  na mshambuliaji wa zamani wa Sunderland, Jermain Defoe amwaga machozi wakati wa kuuaga mwili wa kipenzi chake, shabiki mdogo wa Sunderland, Bradley Lowery kanisa la Mtakatifu Joseph leo kabla ya mazishi yake.
 Bradley alifanywa kuwa kibonzo-nembo wa klabu hiyo na akaunda urafiki wa karibu na mshambuliaji wa klabu hiyo Jermain Defoe.
Aidha, aliongoza wachezaji wa England kuingia uwanjani Wembley wakati wa mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Lithuania.
Jeneza lenye mwili wa Lowery lilisafirishwa kwa kutumia kigari cha farasi kupitia kijiji mwao
Bradley alipewa matibabu lakini saratani yake ikaibuka tena mwaka jana.
Wahisani walichangisha zaidi ya £700,000 kulipia matibabu yake New York mwaka 2016, lakini madaktari waligundua kwamba saratani yake ilikuwa imeenea sana na hangeweza kutibiwa.
 Wazazi wake Gemma na Carl, kutoka Blackhall Colliery, Durham, waliambia Desemba kwamba alikuwa amesalia na "miezi kadha tu ya kuishi".
Miezi minne baadaye, walifahamishwa kwamba jaribio la mwisho kabisa la kumtibu lilikuwa limefeli.
 Bradley alipendwa na maelfu ya watu na alipokea kadi 250,000 za kumtakia heri wakati wa Krismasi mwaka jana, kutoka kwa watu mataifa ya mbali kama vile Australia na New Zealand.

Meneja wa zamani wa Sunderland David Moyes alikuwa miongoni mwa watu mashuhuri katika soka waliohudhuria mazishin hayo
Wengi wa waombolezaji walivalia jezi za Sunderland, kama familia yake ilivyokuwa imewaomba
Waombolezaji waliovalia jezi za Sunderland walipamba barabara kwa maputo na mabango

Post a Comment
Powered by Blogger.