Mtoto wa George Weah asajiliwa PSG


Mtoto wa mshambuliaji hatari kuwahi kutokea barani Afrika, George Weah, Tomothy Weah amesaini mkataba mpya wa kuichezea klabu ya soka ya PSG inayoshiriki ligi kuu ya Ufaransa.
Timothy ambaye alikuwa akiichezea timu ya vijana ya PSG yenye umri wa chini ya miaka 17, amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuichezea timu hiyo ambao utafikia tamati mwaka 2020.
Baada ya kusaini mkataba huo, mchezaji huyo amesema, “Ni fahari kubwa kuendeleza pale baba alipowachia. Niko katika klabu kubwa na natumai nitaendelea kuimarika ili niweze kuichezea timu kubwa.” Nao PSG kupitia matando wao wa Twitter walionyesha furaha yao ya kumsaini kinda huyo kwa kuandika, “PSG proudly announces that Timothy Weah has signed his first professional contract with the club.”

Timothy akiwa na baba take mzazi, George Weah pamoja na Gandhi ya mabosi wa PSG
Timothy ni mtoto wa tatu katika familia ya George Weah wa nchini Liberia ambaye pia amewahi kuwa mchezaji bora wa dunia kwa mara tatu. Weah amewahi kuchezea timu kubwa kadhaa ikiwemo PSG, AC Milan, Manchester City, Monaco, Chelsea na nyingine.
Post a Comment
Powered by Blogger.