Jeshi la polisi kanda maalum ya DSM latangaza operesheni maalum ya kuwabaini wezi wa vifaa vya magari

Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limetangaza operesheni maalum ya kuwabaini wezi wa vifaa vya magari ambapo wafanyabiashara wote ambao wanauza vipuri vya magari vilivyotumika wanatakiwa kuonyesha nyaraka za kuingiza bidhaa zao hapa nchini pamoja na risiti za kodi walizolipia kodi na kama watashindwa kufanya hivyo wataunganishwa na kundi na wezi wa vifaa vya magari.

Operesheni hiyo imetangazwa na kaimu kamanda wa polisi wa kanda hiyo Lucas Mkondya wakati akitangaza operesheni hiyo kwa umma ambapo amesema maduka mengi ya vifaa vya magari vimekuwa vikitumika kama sehemu ya kuuzia vitu vya wizi.

Aidha kamanda huyo amesema watahakikisha wanakomesha mtandao wote wa wezi wa magari na tayari wametuma kikosi maalaum cha polisi nje ya nchi kwenda kubaini mtandao huo wawezi wa magari.

Chanzo: ITV Tanzania
Post a Comment
Powered by Blogger.