Defoe awatoa machozi mashabiki na familia ya Bradley

Bradley Lowery ameshatangulia mbele za haki, pamoja na kupambana na ugonjwa wa kansa uliomsumbua tangu akiwa na mwaka mmoja sasa amekufa akiwa na miaka 6.
Ukiacha familia ya Bradley ambao walikuwa karibu sana na mtoto huyo, mtu mwingine aliyekuwa karibu sana na Bradley alikuwa ni Jermain Defoe.
Defoe amekuwa bega kwa bega na Bradley tangu alipokuwa akiitumikia Sunderland na hata aliposajiliwa kwenda Fc Bournemouth alienda kumuaga Bradley.
Baada ya kifo cha Bradley watu wengi wamekuwa wakituma salamu za rambirambi kwa familia yake wakiwatia moyo katika kipindi hiki kigumu cha msiba.
Jermain Defoe naye ametuma ujumbe mrefu kueleza hisia zake juu ya kifo cha Bradley, ujumbe wa Defoe umewatoa wengi machozi kutokana na maneno ya hisia aliyoandika kupitia ukurasa wake wa Twitter.
Defoe aliandika “Kwaheri rafiki yangu nitakukumbuka sana, najisikia mwenye baraka sana kwa mungu kunikutanisha na wewe katika maisha yangu na kupitia nyakati nyingi pamoja”
Aliendelea “kamwe siwezi sahau tulivyokutana mara ya kwanza na jinsi ulivyoniangalia na macho yako mazuri hakika napata wakati mgumu kuelezea ulivyokuwa muhimu kwangu’
“Nitakumbuka jinsi ulivyokuwa ukilitaja jina langu na jinsi ulivyokuwa ukitabasamu wakati camera zikiwa zinaelekezwa upande wetu, hakika nilifurahia kuwa na wewe.”
“Faraja na ujasiri wako vitazidi kuwa katika akili yangu siku zote za maisha yangu,sasa mungu yuko na wewe mikononi lakini kwangu nitakubeba moyoni mwangu kila saa” alimaliza kuandika Defoe.
Post a Comment
Powered by Blogger.