Picha: Timu ya Uingereza yaweka kambi ndani ya Jeshi lake la Ulinzi

Wachezaji wa timu ya Taifa ya Uingereza wakiwa katika kombati za Jeshi katika kambi yao

Timu ya Uingereza yaweka kambi ndani ya Jeshi lake la Ulinzi
Timu ya Taifa ya Uingereza yaweka kambi katika jeshi lao la ulinzi wa majini ili kujiweka fiti kwaajili ya michezo inayo ikabili kikosi hiko cha simba watatu.
Kikosi hiko kinaamini kuwa kufanya mazoezi ndani ya kambi ya jeshi lao tiifu itawaongezea hamasa na uimara ndani ya timu kuelekea mchezo wao wa Jumamosi wa kuwania kucheza Kombe la Dunia dhidi ya Scotland na kisha kukutana na timu ya taifa ya Ufaransa.

Timu ya Taifa ya Uingereza itaikabili timu ya Scotland Jumamosi wa kuwania kucheza Kombe la Dunia

Wadau wa soka nchini Uingereza walishitushwa wakati meneja wa kikosi hiko , Gareth Southgate kuamuru kambi yao ikafanyike katika kambi za mafunzo ya Comando wa jeshi huko Devon.

Wachezaji 22 wa timu ya taifa ya Uingereza ambao walikuwa mapumzikoni baada ya msimu wa ligi kumalizika walikubaliana na mawazo ya kocha wao kwa kambi ya timu hiyo ipelekwe katika kambi za Jeshi.

Meneja Gareth Southgate akijiunga na kempu

“Tunahitaji kuwapeleka vijana wetu katika mazingira tofauti ambayo wao hawakuyatarajia,”

“Jeshi lilisema tuwafanyie wachezaji wetu kitu ambacho kisicho tarajiwa na hiyo ilikuwa ni moja ya mtazamo wetu wa kambi”. Gareth Southgate aliliambia shirikisho la mpira wa miguu nchini Uingereza FA.

Picha za timu ya taifa ya Uingereza wakiwa kambini
Mshambuliaji wa Man City , Raheem Sterling akiwa katika mazoezi ya nguvu
Mshambuliaji wa Man City , Raheem Sterling akiwa katika mazoezi ya nguvu
Timu ya taifa ya Uingereza wakipata kifungua kinywa nyakati za asubuhi

Post a Comment
Powered by Blogger.