Ushahidi kesi ya Wema Sepetu wakwama kutolewa

Kesi ya kukutwa na dawa za kulevya inayomkabili Wema Sepetu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirishwa hadi Julai 10.
Wema ambaye ni mshindi wa taji la urembo, maarufu Miss Tanzania kwa mwaka 2006 na msanii wa filamu, anakabiliwa na kesi hiyo akidaiwa kutumia na kupatikana na bangi.
Wakili wa Serikali, Elizabeth Mkunde mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa alisema kesi ilipangwa leo (Jumatano) kuanza kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka lakini Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba anayeisikiliza kesi hiyo yupo likizo.
Kutokana na hilo, aliomba iahirishwe hadi Julai 10 ombi lililokubaliwa na mahakama.
Wema na wenzake Angelina Msigwa na Matrida Abbas wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na dawa za kulevya na kutumia dawa hizo.
Inadaiwa Februari 4, katika makazi ya Wema, Kunduchi Ununio, walikamatwa wakiwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08.
Wema pia anadaiwa Februari Mosi katika eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam alitumia bangi.
Post a Comment
Powered by Blogger.