TGNP YAWAKUTANISHA WADAU MBALIMBALI KUJADILI MAPENDEKEZO YA BAJETI YA MWAKA 2017/18

TGNP Mtandao imewakutanisha wadau mbalimbali kutazama nakutoa maoni yao ya bajeti iliyowasilishwa na waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango alipowasilisha Bungeni mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa mwaka 2017/18 Bungeni mjini Dodoma.

Akizungumza kwenye mkutano Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi Lilian Liundi amesema wamewakutanisha wadau hao ili kujadili bajeti pendekezwa ya mwaka 2017/18 iliyowasilishwa bungeni mjini Dodoma.

Alizungumzia bajeti hiyo kwenye mlengo wa kijinsia hasa kwa watoto wa kike wanapokuwa mashuleni na hata kwenye sekta mbalimbali zilivyoguswa na bajeti ya 2017/2018.
Mjumbe wa Bodi ya TGNP Mtandao, Edwin Mhina akitolea ufafanuzi baadhi ya mambo aliyojadiliwa kuhusu hali ya uchumi 2016 na mpango wa maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2017/18 kabla ya kuaza kwa usomaji wa bajeti ya mwaka 2017/18.
Wadau mbalimbali wa Maendeleo waliokutanishwa na TGNP Mtandao wakiendelea kufuatilia Hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango alipokuwa anawasilisha Bungeni mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa mwaka 2017/18 Bungeni mjini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi Lilian Liundi akizungumzia kuhusu kuachwa kwa mtoto wa kike nyuma kwenye bajeti ya mwaka 2017/18 hasa kwenye mazingira mazuri ya mtoto wa kike anapokuwa shule mara baada ya kumalizika kwa Hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango alipowasilisha Bungeni mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa mwaka 2017/18 iliyosomwa Bungeni mjini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa HakiElimu, Godfrey Boniventura akizungunzia bajeti ya elimu iliyopeleka pesa nyingi kwenye elimu ya juu na kutengwa pesa ndogo kwenye shule za mzingi pamoja na sekondari ambapo inasababisha ufanisi wa elimu kushuka hapa nchini.

Baadhi ya wadau mbalimbali waliokutanishwa na TGNP Mtandao ili kuangalia bunge mubashara wakati wa uwasilishwaji wa bajeti wakichangia mada mara baada ya kumalizika kwa Hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango alipowasilisha Bungeni mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa mwaka 2017/18 Bungeni mjini Dodoma.
Post a Comment
Powered by Blogger.