MATANGAZO....
pamoja blogBABA

HABARI

MATUKIO

Michezo imedhaminiwa na

MICHEZO

Simulizi zimedhaminiwa na

SIMULIZI

JAMII

BURUDANI

UCHUMI

MAGAZETI

VIDEO ZETU

» » » » PICHA: MMILIKI WA IPTL, MFANYABIASHARA JAMES RUGEMALILA WAFIKISHWA MAHAKAMANI


Pamoja Blog 6/19/2017 10:00:00 PM 0

 James Rugemalila na mmiliki wa Kampuni ya IPTL, Harbinder Seth Sigh, wakiwa chini ya ulinzi wa Polisi kabla ya kupanda kizimbani.  (Picha na Francis Dande)

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imewafikisha mahakamani, mmiliki kampuni ya PAP, Habirnder Seth Singh na mfanyabiashara James Rugemalira kwa makosa ya uhujumu uchumi.
Akizungumza na waandishi wa habari, leo Jumatatu, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Kamishna Valentino Mlowola amesema, “Leo nawapa taarifa kuwa tunawafikisha mahakamani watuhumiwa wawili, kwa makosa ya kuhujumu uchumi na mengine yanayofanana na hayo.”
Amesema kwa muda mrefu amekuwa akiulizwa kesi za Escrow na kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) zimeishia wapi, hivyo taasisi hiyo imechunguza shauri hilo kwa muda mrefu na kujiridhisha kwamba linaweza kufikishwa mahakamani.
“Kwa hatua ya awali wataenda Mahakama ya Kisutu, baada ya hapo kuna utaratibu wa kimahakama, watapelekwa mahakama maalumu kutokana na kiwango cha hujuma kilichofanyika na fedha zilizohusika,” amesema Mlowola.
James Rugemalila na Harbinder Seth Sigh, wakinyanyuka kuelekea mahakamani.
 Mke wa mfanyabiashara maarufu, James Rugemalila (wa pili kushoto) akiwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, wakati mume wake alipofikishwa mahakamani kwa kosa la uhujumu uchumi pamoja na mmiliki wa Kampuni ya IPTL, Harbinder Seth Sigh.
 Watuhumiwa wa kesi ya uhujumu uchumi, Mfanyabiashara, James Rugemalila na mmiliki wa Kampuni ya IPTL, Harbinder Seth Sigh wakiwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
Familia ya Rugemalila ikifuatilia mwenendo wa kesi hiyo mahakamani.

 James Rugemalila akiwa chini ya uliunzi wa Polisi wakati akitoka mahakamani.
 Watuhumiwa wa kesi ya uhujumu uchumi, mfanyabiashara, James Rugemalila na mmiliki wa Kampuni ya IPTL, Harbinder Seth Sigh wakitoka mahakamani.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments