Lowassa awasili makao makuu ya polisi, Ulinzi Waimarishwa Barabara Zote

Msafara wa Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa ukiwa na magari manne ukisindikizwa na magari mawili ya polisi umewasili makao makuu ya polisi.

Jana Lowassa alipewa taarifa ya kwenda  kuhojiwa kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).

Mapema leo, Jumanne asubuhi polisi wameimarisha ulinzi katika barabara zote zinazoingia Makao Makuu ya Jeshi la Polisi yaliyopo Mtaa wa Ohio.

Polisi wakiwa na silaha wameegesha magari yao kwenye kila barabara inayoingia makao makuu ya jeshi hilo, huku wengine wakizunguka zunguka maeneo ya jirani.

Wananchi wanaruhusiwa kupita lakini walio kwenye vikundi wanasimamishwa na kuhojiwa, huku wengine wakizuiwa kabisa kukatiza eneo hilo.
Post a Comment
Powered by Blogger.