HALI YA MTOTO BRADLEY LOWERY YABADILIKA GHAFLA

Nilipost habari zake mwezi February juu ya taarifa ya madaktari kueleza kwamba ataishi kwa masaa 24 tu, Lakini miezi minne baadae Lowery ameendelea kuishi na kansa iliyosambaa katika mwili wake.
Lowery amekuwa maarufu kwa sababu ya mapenzi yake kwa timu ya Sunderland na timu ya taifa ya Uingereza. Mwezi Decemba alipewa heshima ya kupiga penati kabla ya kuanza kwa mchezo kati ya Sunderland dhidi ya Chelsea. Tangu hapo kulianzishwa kampeni maalumu ambapo zilikusanywa paundi za Uingereza takribani £700,000 sawa na bilioni 1.9 (shilingi za Tanzania), Lakini haikusaidia kitu kwani uchunguzi wa Madaktari bingwa walieleza hali yake haitibiki.

Wiki hii tena Familia yake imeripoti kuwa hali ya Bradley Lowery ni mbaya, na pengine ndani ya wiki moja hawatakuwa nae. Hii ni mara ya pili baada ya ripoti ya namna hiyo iliyotolewa Mwezi februari mwaka huu. 
Kwa sasa Lowery yupo katika hali mbaya ya maumivu na mzunguko mdogo wa hewa ya Oksijeni kwani kansa hiyo inayoitwa ‘neuroblastoma’ imemtesa tangu akiwa na miaka miwili(Kwa sasa ana miaka 6)
Mwezi uliopita Lowery alipewa heshima ya ‘Child of Courage’ wakati wa tuzo za Pride of North East. Pia alipewa nafasi ya kuongoza wachezaji wa timu ya Uingereza kuingia Uwanjani kupambana na timu ya taifa ya Lithuania. Yeye aliingia uwanjani akiwa na tabasamu tu. Ingawa ukweli ni kwamba ni mgonjwa.

Mama yake ameeleza wiki hii maumivu anayojisikia kujua kwamba mwanae sasa yupo katika nyakati zake za mwisho. Bradley amepokea kadi laki 2 na elfu 50 (250,000) toka ulimwenguni kote zikimtakia afya njema. Tayari familia ya Bradley imekuwa ikijiandaa kwa ajili ya tukio muhimu linaloelezwa kutokea ndani ya wiki moja tu ijayo ingawa ya Mungu mengi naye huamua jambo kulingana na matakwa yake.

Francis Daudi,
Brookefield.
Post a Comment
Powered by Blogger.