Fahamu Biashara tano unazoweza kuzifanya ukiwa mkoa wa Dar es Salaam

Dar es Salaam kuna changamoto nyingi endapo hauna shughuli maalumu ya kufanya basi lazima utauchukia mji huu na kuona sio sehemu sawa kwa wewe kuwepo, ila ukifanikiwa kujua cha kufanya ukiwa hapa basi lazima utaona Mkoa huu ni mrahisi sana.Zifatazo ni biashara za kufanya ukiwa hapa.

Biashara ya kwanza :-Kuuza vinywaji baridiJiji la Dar es Salaam limekuwa na asili ya kuwa na joto sana hivyo ni rahisi kwako wewe kuifanya biashara ya vinywaji baridi kama soda, maji na juisi hasa maeneo yenye pilika piliaka za watu na uhitaji wa vitu hivyo mara zote. Mfano unaweza kuuza katika eneo la soko, maeneo ya vituo vya basi pamoja na wakati wa foleni barabarani.

Biashara ya Pili : -Kuuza magazeti

Mara nyingi kumekuwa na uhitaji wa watu wa kupata habari, sio wote wenye simu wanajua njia za kupata habari na sio wote wanakuwa na uwezo wa kununua bando ilikuweza kuperuzi mitandao kujua kinachoendelea, hivyo bado kuna uhitaji wa magazeti ukizingatia wengi wanakuwa busy na shughuli zao.Kupita kusoma gazeti ndiyo huwa muda pekee wao kujua mambo yananayoendelea na husoma magazeti hasa kwenye foleni za magari asubuhi wanapokwenda na jioni wanaporudi kwenye shughuli zao.

Biashara ya tatu ;- Uuzaji wa matunda


Kiafya ni moja ya hitaji kubwa sana katika mwili wa binadamu, hivyo biashara hiyo ni nzuri kuifanya ukiwa hapa na biashara hii ubadilika badilika kulingana na msimu wa tunda husika. Mtaji wa biashara hii ni mdogo na sehemu nzuri za kupatia wateja ni kwenye vituo vya mabasi, pembezoni mwa barabara, karibu na migahawa au karibu na ofisi.

Biashara ya nne ;- Uuzaji wa vocha ama muda wa maongezi

Japo imelalamikiwa kutokuwa na faida ila mkaa bure sio sawa na mtembea bure, Wakazi wengi wa jiji hili hutumia vocha kurahisha shughuli zao kwa kuwasilana na ndugu, jamaa ana rafiki. Hii hupelekea wanaouza vocha za muda wa maongezi kuwa na uhakika na biashara zao.

Biashara ya tano :- Uuzaji wa chakula.Hapa ndiyo patamu sasa, kila mtu napenda kula, Biashara ya kuuza chakula ni nzuri kwani binadamu yoyote anahitjika kupata chakula.Lakini sio chakula tu hata vyakula vya baharini, kama pweza ni moja ya vitu vinavyoweza kukufanya ukaendela kuwepo hapa mjini.Pia biashara ya chakula aina ya chips ni nzuri pia kwani inawateja wengi.

MUHIMU:

Unatakiwa ujue kuwa kila biashra inachangamoto zake hivyo cha msingi ni kukabiriana nazo iliuweze kufika malengo yako.

Na Laila Sued
Post a Comment
Powered by Blogger.