CRISTIANO RONALDO AONYESHA UPENDO KWA MTOTO MLEMAVU

Cristiano Ronaldo amesababisha furaha kwa mtoto mlemavu aliyekuwa akiwasindikiza wachezaji wa Ureno uwanjani akiwa kwenye kiti cha matairi katika mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Urusi.

Kapteni huyo wa Ureno alimfanya mtoto huyo wa kike uso wake kujawa na tabasamu kubwa wakati alpokuwa akiingia naye uwanjani kutoka kwenye lango la kuingilia wachezaji la katika uwanja wa Spartak Jijini Moscow.

Katika hali ambayo iliamsha hisia za wengi ni pale wachezaji wa Ureno wakijiandaa kwa wimbo wa taifa Ronaldo alimpa mtoto huyo jaketi lake la mazoezi na kisha akambusu katika paji lake la uso.
                  Cristiano Ronaldo akimpa jaketi lake la mazoezi mtoto huyo mlemavu 

   Mchezaji nyoto wa Ureno Cristiano Ronaldo akimbusu kwenye paji la uso mtoto mlemavu
Post a Comment
Powered by Blogger.