CHELSEA YAANZA KUWAUZA VIJANA WAKE KUSAKA FEDHA ZA USAJILI WA BAKAYOKOTimu ya Chelsea imeanza kuwauza wachezaji wake ili kuwanunua Tiemoue Bakayoko na Alex Sandro, ambapo sasa wamekuja na mbinu ya kuweka sharti la kuruhusiwa kuwanunua tena wachezaji vijana inaowauza.Tayari mchezaji wa Chelsea, Bertrand Traore, amehamia Lyon ya Ufaransa kwa kitita cha paundi milioni 16 hapo jana, ambapo Chelsea itapata asilimia 15 ya faida iwapo Lyon itaamua kumuuza baadaye.Timu ya Chelsea pia imeweka kifungu cha kumnunua tena itakapomuhitaji ili kuepusha kosa walilolifanya kwa Romelu Lukaku, pia beki Nathan Ake anayewaniwa na Bournemouth kwa kitita cha paundi milioni 20 amewekewa kifungu hicho.
                                     Bertrand Traore akiwa ameshatua rasmi katika timu ya Lyon
Chelsea ilimuuza Romelu Lukaku kwa Everton kwa kitita cha paundi milioni 28 bila kifungu cha kuweza kununua tena
Post a Comment
Powered by Blogger.