Wafanyabiasha Mwanza watishia kugoma

Wakazi wa jiji la Mwanza huenda wakakosa huduma katika masoko 14 jijini humo baada ya wafanyabiashara kutangaza mgomo ifikapo Julai 4, mwaka huu iwapo malalamiko na hoja zao kuhusu ongezeko la kodi ya vyumba na vizimba vya biashara hayatapatiwa ufumbuzi.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake zaidi ya 2000, mwenyekiti wa wafanyabiashara hao, Hamad Nchola alitaja kitendo cha wamachinga kuruhusiwa kupanga bidhaa zao pembezoni mwa maduka na vizimba vyao kuwa miongoni mwa sababu za mgomo wao.

Nchola alitaja kitendo cha maduka ya wenzao 40 wa soko la Buzuruga kufungwa na Mali zao kuchukuliwa na halmashauri Manispaa ya Ilemela inayounda Jiji la pamoja Nyamagana kuwa miongoni mwa sababu za mgomo wao usio na kikomo.

Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba alisema ofisi yake haijapokea taarifa za tishio la mgomo wa wafanyabiashara hao.
Hata hivyo, Kabamba alisema mara kadhaa uongozi wa jiji umekutana na wafanyabiashara hao kujadili na kutafutia ufumbuzi changamoto zinazowakabili.

Chanzo: Mwananchi
Post a Comment
Powered by Blogger.