UPDATES: WANAFUNZI 31 NA WALIMU WAO WADAIWA KUPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI YA GARI WILAYANI KARATU LEO

Kamanda wa Polisi, mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amesema wanafunzi 31 na walimu wao wamefariki katika ajali iliyotokea wilayani Karatu, ulipo mto Mlera.
Mkumbo amesema wanafunzi waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni wa shule ya mchepuo wa Kiingereza, iitwayo Luck Vicent ya mjini Arusha.
Kati ya wale waliofariki 28 walikuwa wanafunzi huku watatu wakiwa ni dereva na walimu wao
Ripoti zinasema kuwa basi hilo liliteleza na kukosa mwelekeo ,likatoka katika barabara na kuanguka katika mto katika eneo la Marera eneo la Rhotia, kilomita chache kabla ya karatu katika barabara ya Arusha
Zoezi la uokoaji likiendelea.
Post a Comment
Powered by Blogger.