Update: Majeruhi wa Lucky Vicent wanaotibiwa Marekani, Mmoja atoka nje kwa mara ya kwanza

Doreen mara baada ya upasuaji
Majeruhi wa ajali ya basi la wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent waliopelekwa kutibiwa nchini Marekani, inaripotiwa hali zao kuendelea vizuri huku mtoto mmoja kati yao, Wilson, kwa mara ya kwanza ametoka nje.
Taarifa iliyotolewa na Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, imeeleza kuwa Mtoto Doreen amemaliza kufanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo, kwa kile ambacho madaktari wamesema kumefanikiwa kwa ufanisi mkubwa, kupita matarajio yao. Doreen alikuwa afanyiwe upasuaji kwa makadrio ya masaa 5:30, lakini zoezi hilo lilikamilika kwa muda wa masaa 4:00, huku timu ya “Surgical Support” ikiwa na watu sita, na kwa pamoja wakiongozwa na madaktari bingwa wawili, Dr. Meyer na Dr. Durward.
Doreen amehamishwa kutoka chumba cha upasuaji na kupekewa ICU, na madaktari wamesema kwa kuwa hali yake imeridhisha sana, baadae leo watamtoa ICU ambako wamempumzisha baada ya upasuaji, na kumrudisha wodi ya watoto ambako ataendelea na mapumziko. Mungu amesikia maombi ya Watanzania na wote waliotoa Sala na Dua zao kwa ajili ya Mtoto Doreen popote Duniani.

Mtoto Wilson kwa mara kwanza ametoka nje ya Jengo Kuu la Hospital ya Mercy akiwa kwenye “wheelchair”, huku Mama na Daktari wake wakiwa na tabasamu.
Post a Comment
Powered by Blogger.