Safari ya Himid Mao kutimkia Ulaya imekwiva

Mchezaji wa Azam FC, Himid Mao

Kiungo wa Klabu ya Azam FC, Himid Mao ambaye mwanzoni mwa mwezi huu alienda nchini Denmark kufanya majaribio na Klabu ya Randers FC, ndoto ya kiungo huyo ya kucheza soka la kulipwa ipo karibu kutimia kwani mabosi wa Klabu hiyo na wa Azam FC wamekutana jijini Dar es salaam kufanya mazungumzo ya mwisho kuhusu usajili wake.
Hatua hiyo imekuja baada ya Himid kufuzu majaribio ya siku 10 aliyoenda kufanya katika timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Denmark, mapema mwezi huu.
Ofisa Habari wa Klabu ya Azam FC, Jaffar Idd amesema kuwa kwa sasa wapo kwenye mazungumzo na mabosi hao wa Randers baada ya kuwapa habari kwamba kiungo wao amefuzu majaribio yake.
Tupo kwenye majadiliano na wao, tunasubiri kusikia ofa yao na kama tukikubaliana basi Himid ataenda kujiunga nao kwa sababu wametuambia tayari amefuzu, hivyo mazungumzo yaliyopo sasa ni baina yao na sisi”, alisema Jaffar Idd kwenye mahojiano yake na Gazeti la Championi.
Kwa upande mwingine Kocha wa Azam FC, Aristica Cioaba amesema kuwa kama dili hilo litafanikiwa, basi anamtakia kila la heri kiungo huyo.

Post a Comment
Powered by Blogger.