MATANGAZO....
pamoja blogBABA

HABARI

MATUKIO

Michezo imedhaminiwa na

MICHEZO

Simulizi zimedhaminiwa na

SIMULIZI

JAMII

BURUDANI

UCHUMI

MAGAZETI

VIDEO ZETU

» » » » Mwanafunzi wa UDOM akutwa na misokoto 826 ya bangi


Pamoja Blog 5/12/2017 12:21:00 PM 0

Jeshi la polisi mkoani Dodoma linawashikilia watu wawili kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi akiwamo mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) Nelson Matee (24) ambaye ni mwanafunzi wa kozi ya uuguzi mwaka wa nne.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake leo asubuhi, kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa alisema kuwa mwanafunzi huyo alikamatwa Mei 9 mwaka huu kufuatia msako mkali uliofanywa na jeshi hilo chuoni hapo ambapo mtuhumiwa alikutwa na jumla ya misokoto 826 ya bangi yenye uzito wa kilo 2.8 akiwa ameiweka kwenye mifuko ya nailoni chumbani kwake.

Mambosasa amesema kuwa mtuhumiwa alipohojiwa alisema kuwa amekuwa akifanya biashara hiyo ya kuuza bangi kwa kipindi cha miaka minne tangu alipojiunga na chuo hicho na kwamba alikuwa akiwauzia wanafunzi wenzake.

Chanzo: Mwananchi

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments