MATANGAZO....
pamoja blogBABA

HABARI

MATUKIO

Michezo imedhaminiwa na

MICHEZO

Simulizi zimedhaminiwa na

SIMULIZI

JAMII

BURUDANI

UCHUMI

MAGAZETI

VIDEO ZETU

» » » Man City marufuku kusajili miaka miwili


Pamoja Blog 5/06/2017 03:38:00 PM 0

Klabu ya soka ya nchini Uingereza, Manchester City, imefungiwa kusajili na bodi ya ligi ya nchini hiyo vijana wadogo walio na umri wa chini ya miaka 18 sambamba na kutozwa faini ya Paundi 300,000 kwa kuvunja sheria ya maendeleo ya vijana.
Kufuatia uchunguzi wa Bodi ya Ligi Kuu, ushahidi umepatikana kwa City wamevunja sheria za Ligi.

Uvunjaji huo wa sheria unahusu kufanya mazungumzo na wachezaji wawili wa academy tofauti kwa ajili ya kuwasajili huku wakiwa wamesajiliwa na klabu nyingine.
Adhabu hiyo ni sawa na waliyopewa Liverpool mwezi uliopita baada ya kukutwa na hatia ya ‘kuiba’ mchezaji mwanafunzi wa shule wa Stoke City.
Kuwasiliana na mchezaji wa academy yoyote akiwa amesajiliwa na klabu yake ya wakati husika ni kosa, ambalo City wamefanya na sasa linawagharimu.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments