ACACIA WAJIPANGA KUUFUNGA MGODI WA BULYANHULU WANAOUITA "LOSS MAKING MINE":

Kwa mujibu wa gazeti la The Telegraph la Uingereza, kampuni ya Acacia inajiandaa kuufunga mgodi wake wa Bulyanhulu, kampuni hiyo imedai mgodi huo umekuwa ukizalisha hasara licha ya ripoti iliyoundwa na Rais Magufuli kubaini udanganyifu mkubwa wa kiwango cha dhahabu na madini mengine yaliyokutwa kwenye makinikia yaliyokuwemo kwenye makontena 277 yaliyozuiliwa na serikali.
Kampuni ya Acacia inadai kupata hasara ya Dola Milion 1 (zaidi ya Tshilling Bilion 2) kila siku kutokana na zuio la serikali. Kampuni hiyo inadai kushangazwa na kiwango kikubwa kilichotajwa na kamati hiyo, Acacia wanadai endapo kiwango kilichotajwa na kamati ni sahihi basi mgodi utakuwa mgodi wa tatu kwa ukubwa duniani.

Source: The Telegraph
Post a Comment
Powered by Blogger.