Sipendi maisha ya Ustaa - Madam Flora

Madam Flora (zamani Flora Mbasha) amesema hayo hivi karibuni ikiwa ni siku chache kuelekea ndoa yake ambapo amefunguka na kudai kuwa baada ya kumpata mwanaume ambaye siyo maarufu anafurahi kwani hata mfumo wa maisha yake utaenda kubadilika na kuishi kama watu wengine ambao siyo maarufu.

"Mume wangu mtarajiwa siyo mtu anayejulikana bali naamini kwenye ulimwengu wa kiroho anajulikana. Namshukuru Mungu maisha mapya ambayo naenda kuyaishi siyo ya umaarufu. Mimi nimemwambia pamoja na ustaa nilionao napenda tuishi maisha ya kawaida ambayo hayahusiani na umaarufu wangu. Unajua kuna wakati natamani kushuka kwenda kula chakula kwa mama n'tilie lakini watu watashangaa hata wewe? sasa najiuliza who is Flora? kumbe mimi pia ni mtu wa kawaida kabisa. Sitamani maisha ya Ustaa yananinyima uhuru"- Madam Flora.

Aidha Flora amefunguka kuhusu mahusiano yake na kwamba kabla ya kukubali kuolewa kwa mara ya pili ilimchukua zaidi ya mwaka mmoja kutafakari ikiwa ni pamoja na kushirikisha familia kwa ajili ya maombi. "Mimi na David tuna miaka miwili na nusu ya urafiki wa kawaida lakini aliponiambia kuhusu suala la ndoa nilikaa mwaka mzima kutafakari kwa sababu nilikuwa natamani mwanaume atakayeniheshimu, kunijali na kunipenda na yeye vyote anavifanya. Hata hivyo namshukuru Mungu kwa kurudi nyumbani ingawa sikuwa nawaza kama nitapata mume Mwanza lakini ndo imetokea.

Katika hatua nyingine Flora amezungumzia ugumu wa kubadilisha jina lake la awali (Flora Mbasha) hadi kufikia kulikubali jina la Madam Flora huku akishukuru kwa kuwa limeshaanza kuzoeleka kwa baadhi ya watu na hata watumishi wa Mungu. Flora anatarajiwa kufunga ndoa na Mwanaume aliyemtaja kwa jina moja la David kesho mkoani Mwanza baada ya ndoa yake na Muimbaji wa nyimbo za injili Emmanuel Mbasha kupeana talaka.
Post a Comment
Powered by Blogger.