SAKATA LA ROMA : WASANII WAINGIWA NA HOFU KUU, WAFUNGUKA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII

Ni siku ya pili sasa, Roma, Moni Centrozone, producer wa Tongwe Records, Bin Laden na vijana wengine waliotekwa na watu wasiojulikana walipokuwa katika studio hizo, bado haijafamika walipo.

Jitihada za awali zilizofanywa na watu wao wa karibu, akiwemo mke wa Roma,Nancy zimegonga mwamba. Katika mahojiano na vyombo mbalimbali vya habari, Nancy amesema amezunguka katika vituo vingi vikubwa vya polisi kuulizia taarifa za mumewe jibu analokutana nalo ni ‘hatuna taarifa zozote, tutashughulikia.’ Majibu hayo hayana matumaini kwa Nancy ambaye ni siku ya pili sasa hajamuona wala kusikia sauti yake mume wake aliyemuuaga usiku wa juzi kuwa anaenda Tongwe Records, studio ambayo hurekodi nyimbo zake.
“Serikali, waandishi wa habari, Watanzania, yeyote aliyeona, aliyesikia, anayeweza kutusaidia Roma yuko wapi naombeni msaada wenu,” anasema Nancy ambaye yeye na Roma wamebarikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume, Ivan.
“Nahitaji kufahamu yuko wapi, yuko katika hali gani,” anaongea kwa uchungu.
Roma na wenzake wako wapi? Ni swali ambalo kila mtu anajiuliza kwa sasa? Wasanii wengi wameingiwa na hofu kubwa. Haya ni baadhi ya maoni yao:

Vanessa Mdee
Wherever you are, God is Bigger than, Stronger than, Realer than all the other forces that be. Stay UP brother @roma2030 #VivaRoma #FreeRoma #FreeMoni roho inauma na nimetoka kumsikiliza mkeo redioni hajui hata ulipo sasa ndiyo nini ๐Ÿ˜ก๐Ÿ˜ก๐Ÿ˜ก๐Ÿ˜ก๐Ÿ˜ is this where we are at now? Ma studio yanavamiwa, watu wanakamatwa kama wanyama pori. Aaaarrrrgh

Diamond
Wakati mwingine natafakari sijui hata wapi tunaelekea… lla kwakuwa Mwenyezi Mungu ndio Mpangaji wa yote basi naamini hata hili litapita tu… Mwenyezi Mungu aipe nguvu familia ya @roma2030 na wanamziki wenzetu wote ambao hadi sasa haijajulikana walipo..

Nay wa Mitego
Siku nzima ya leo nimekosa raha kabisa, cjui Mshkaji wangu Yupo kwenye hali gani, mazingira gani.? Roma yuko wapi.?! Sim yake ukipiga inaita Kama kawaidi, Masege Whatsup zinasomwa, Sim hazipokelewi. Vyombo husika tunaomba mtusaidie, tunaitaji kujua ndugu zetu wako wapi.? Hatuwezi kukaa kimya.
Hivi kweli tumefikia huku.? Tunaenda wapi.? #FreeRoma✊๐Ÿฟ
#Wapo


Professor Jay
Wakati sisi tunakosa Usingizi na kuendelea kupaza Sauti, Kuna wengine wameweka miguu juu wanaona hili haliwahusu na wengine wanakwenda mbali zaidi na kudiriki kusema hii ni KICK ya Muziki tu..
Narudia tena kuwaambia ndugu zangu WAKIMALIZANA NA SISI WATAKUJA KUMALIZANA NA NYINYI๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ
#Bring Back our SOLDIERS Alive.

Ray C

Nimeanza kuingiwa na woga,nafikiria mambo mengi Roma alipo Sasa,anafanywa nini na tatizo ni nini mpaka imekuwa hivi na masaa yanaenda hakuna jibu lililo kamili!!hisia mchanganyiko na zote sio nzuri….Nini kinaendelea?Tatizo ni nini??Sababu ni nini?Bado najiuliza sipati jibu………

Fid Q
Nimeipokea hii HABARI kwa mstuko mkubwa.. sio tu kwasababu TONGWE ni moja kati ya wadhamini wetu wa #OpenMicThursday pia ni moja kati ya studio ambazo zimekua msaada mkubwa sana ktk kunyanyua vipaji na C E O @j_murder_tongwe amekua mstari mbele sana ktk kufanikisha hilo.. kinachonistua na kuninyima raha zaidi ni hili la hawa ndugu zetu akina @roma2030 @moni_centrozone Producer Belo na mlinzi kuwa hawajulikani waliko hadi hivi sasa.. ninaiomba MAMLAKA HUSIKA ya USALAMA itusaidie ili waweze kupatikana mapema na kuifutilia mbali ile hofu iliyotanda mioyoni mwa ndugu, jamaa na marafiki… mwisho namuomba MUWEZA WA VYOTE azifanyie wepesi familia za ndugu zetu waliopotelea kusikojulikana in sha Allah

AY
Vyombo husika vifanye uchunguzi wa haraka tujue hali za wasanii wenzetu wako kwenye hali gani..@romamkatoliki Mungu yupo pamoja nanyi awaepushie lolote baya.. @tongwerecords @j_murder_tongwe
Post a Comment
Powered by Blogger.