Mtoto Asombwa na Maji ya Mto Ngerengere Chalinze

MTOTO wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Ubena, Tarafa ya Chalinze mkoa wa Pwani aliyefahamika kwa majina ya Karim Salum, anasadikika kufariki dunia baada ya kuzama kwenye maji ya mto Ngerengere wakati akiogelea na wenzake huku jitihada za kutafuta mwili wake zikigonga mwamba kutokana na wananchi kuutafuta mwili huo kwa zaidi ya siku mbili mfululizo bila mafanikio.

Chanzo kimeshuhudia wananchi wakiendelea na jitihada za utafutaji wa mwili wa mtoto Karim Salum anayesadikiwa kufa maji huku vijana walioshuhudia mtoto huyo akizama ndani ya maji wakieleza tukio hilo lilitokea majira ya saa kumi Alasiri wakati wakijaribu kuogelea ndani ya mto huo.

Naye Babu wa mtoto huyo Bwana Issa Bung’ombe ameeleza kusikitishwa na tukio hilo na kwamba mtoto huyo aliaga nyumbani akielekea mtoni kuchota maji ndipo kadhia hiyo ilipomkuta.
Post a Comment
Powered by Blogger.