Mchekeshaji Charlie Murphy afariki dunia

 Kaka wa Eddie Murphy, Charlie ambaye na yeye pia ni mchekeshaji amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 57.

Kwa mujibu wa meneja wa marehemu, Charlie amefariki jana Jumatano asubuhi katika hospitali ya mjini New York kutokana na ugonjwa wa leukemia.
Charlie amewahi kuigiza kwenye filamu takribani 29 huku filamu yake ya mwisho kuonekana ilikuwa ni ‘Meet The Blacks’ iliyotoka mwaka jana. Lakini pia amewahi kushiriki katika uandishi wa baadhi ya filamu za mdogo wake Eddie Murphy ikiwemo “Norbit” na “Vampire in Brooklyn.”
Muigizaji huyo amefanikiwa kupata watoto watatu ambapo wawili kati yao alizaa na mkewe Tisha Taylor aliyefariki Disemba mwaka 2009 kwa ugonjwa wa kansa.
Post a Comment
Powered by Blogger.