HISTORIA FUPI YA RICE COOKER:

Na Governor Moses Mutente,
Wagunduzi wa kifaa cha kupikia mchele maarufu kama Rice Cooker ni miongoni mwa wagunduzi bora zaidi duniani. Rice Cooker inapendwa na vijana mabachela pote duniani. Rice Cooker ya kwanza ilibuniwa na waanzilishi wa kampuni ya Sony ikiwa ndiyo bidhaa yao ya kwanza kutengeneza. Mwaka 1945 baada ya vita ya pili ya dunia, Japan ilijikuta ikiwa na viwanda vingi vyenye umeme wa kutosha lakini pia kulikuwa na upungufu mkubwa wa fedha hali iliyopekelea watu kutumia mchele kama njia ya malipo. 

Waanzilishi hao wa Sony bwana Ibuka na Morita wakaona fursa na kuamua kutengeneza kifaa cha umeme cha kupikia wali/ubwabwa. Kifaa hicho kilikuwa cha mbao lakini kwa bahati mbaya hakikupika vizuri na mara nyingi wali ulitoka ukiwa haujaiva vyema.

Mwaka 1955 Bwana Yoshidata Minami aliyekuwa akifanya kazi na kampuni ya Toshiba alibuni Rice Cooker yakwanza yenye sifa ya kujisimamia yenyewe yaani "automated". Leo hii makampuni mengi ya kutengeneza Rice Cooker wanatumia design hiyo ambayo vijana tunaipenda kwelikweli. Nchini Japan asilimia 95 ya nyumba zinatumia kifaa hicho. Pichani ni Rice Cooker ya kwanza dunuani iliyotengenezwa na SONY.
Nimejaribu kueleza historia kwa ufupi tu.
Post a Comment
Powered by Blogger.