Wanafunzi wa awali Pongwe jijini Tanga watoroka shule kwa kukosa uji

Wanafunzi walioandikishwa kuanza darasa la awali katika shule mbali mbali za msingi zilizopo kata ya Pongwe jijini Tanga,wanalazimika kutoroka shuleni kwa sababu ya kukosa uji hatua ambayo imewaathiri kitaaluma wanapokuwa darasani.
ITV imeshuhudiia baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Ziwani wakiwa nje huku wakigombea kukinga maji ya bomba lililopo nje ya shule kwa kutumia viganja vya mkono kwa ajili ya kunywa  hatua ambayo imesababisha mwalimu mkuu msaidizi wa shule hiyo Anjelina Mponji kuelezea bayana changamoto zinazowakabili. 

Kufuatia hatua hiyo Diwani wa kata ya Pongwe Mbaraka Salim amesema yeye kama mwakilishi wa wananchi wa kata hiyo atalishughulikia suala hilo ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha wazazi waweze kuchangia kiasi cha fedha kwa ajili ya kuwapikia watoto wao uji shuleni ili waweze kupenda kwenda shule. 
Post a Comment
Powered by Blogger.