Wanafunzi 2,348 washinda rufaa za mikopo ya elimu ya juu

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetuma vyuoni majina ya wanafunzi 2,348 walioshinda rufaa zao na inaendelea kukamilisha malipo ya mikopo yao.
Hatua hiyo ya bodi ya mikopo imekuja baada ya wanafunzi hao kushinda katika rufaa zao za mikopo ya elimu ya juu walizokata tangu Novemba Mosi mwaka jana na kuhitimishwa Januari 31, mwaka huu.
Taarifa ya bodi hiyo iliyotolewa leo (Jumatano) imewaarifu waombaji na umma kwa ujumla kuwa zoezi hilo limefungwa rasmi hadi hapo litakapotangazwa tena katika mwaka ujao wa masomo.
Post a Comment
Powered by Blogger.