Tunda Man kusaidia wasanii wachanga, aanza na msanii aitwae Asala

Msanii mkongwe wa muziki Tunda Man ameweka wazi mpango wake wa kuanza kuwasaidia wasanii wachanga ambapo amenza na msanii mpya aitwae Asala.

Akizungumza na Bongo5 wiki hii, Tunda amedai kwa ukongwe alionao kwenye muziki anaweza kumfundisha muziki hata msanii asiyeweza kuimba na akafanya vizuri.

"Huyu dogo ni kama ndugu yangu na alikuwa ana ndoto ya kufanya muziki muda mrefu, kila wimbo anaoleta namwambia hapana lakini alivyoleta huu wimbo Subiri nikaona kuna kitu kipya kwenye wazo lake. Kwa hiyo nikampeleka kwa studio tukarekodi, tukashoot video na kweli kitu ambacho tumekipata ni kizuri sana hata mashabiki nadhani wamepata kitu tofauti," alisema Tunda.

Aliongeza, "Kwa sasa Asala nipo naye, ni kama ndugu, najaribu kumwelekeza chakufanya na kumwonyesha njia. Mpango wa kusimia wasanii ninao hata kuna wakati niliongea na Madee nikamwambia umri unaenda tutafute vijana tuwasaidie ingawa tupo bado ni Tip Top, lakini lazima tutengeneze vijana wapya ambao watatuwakilisha,"

Tunda amewataka mashabiki wa muziki kupenda muziki mzuri bila kuangalia nani aliyefanya.

Kwa upande wa Asala, alisema anashukuru Tunda Man kwa kumwonyesha njia kwani mpaka sasa tayari ameanza kuona mwanga kwenye muziki wake.

Kwa sasa muimbaji huyo anafanya vizuri na video ya wimbo wake mpya 'Subiri' akiwa amemshirikisha Tunda Man.
Post a Comment
Powered by Blogger.