Rais Magufuli aanza ziara ya siku 4 mikoa ya Kusini

Rais John Magufuli, leo (Alhamisi) ameanza ziara ya kikazi ya siku 4 katika mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara.
Katika ziara hiyo Rais Magufuli atafungua miradi mbalimbali ya maendeleo na kuzungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara.
Leo asubuhi ataweka jiwe la msingi la kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd kilichopo Mkuranga mkoani Pwani na baadaye ataelekea mkoani Lindi.
Kesho ataendelea na ziara yake mkoani Lindi na keshokutwa ataelekea Mtwara.
Post a Comment
Powered by Blogger.