NAPE NNAUYE: KITENDO KILICHOFANYWA NA MKUU WA MKOA KIMENAJISI TASNIA YA HABARI

 Waziri Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye amesema kuwa Tukio la Uvamizi wa Kituo cha Habari cha Clouds unaodaiwa kufanywa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul makonda akiwa na askari kadhaa ni tukio la kupingwa huku akidai kuwa matukio kama hayo hutokea pindi nchi inapotaka kupinduliwa lakini kama Rais yupo, nchi haijapinduliwa.
Aidha amesema kuwa Vitendo hivyo ni kunajisi uhuru wa habari na kama akishindwa kusimamia hilo na yeye hafai kuwa katika nafasi aliyopo.

Chanzo : Mwananchi
Post a Comment
Powered by Blogger.