MWILI WA DEREVA BODABODA WAKUTWA MTO RUVUMA BAADA YA KUPOTEA KWA SIKU 12.

Hali ya taharuki imejitokeza baada ya awali kuelezwa kuwa mwili wa mwendesha boda boda Kasim Njovu aliyepotea kwa siku 12 umeonekana kwenye msitu wa JWTZ Ruhuwiko ambapo wananchi walikusanyika huku wanajeshi na askari polisi wakiutafuta mwili huo bila mafanikio hadi ulipokutwa ukielea kwenye mto Ruvuma katika kijiji cha Litapwasi.
Askari polisi wamelazimika kutishia kufyatua mabomu ya machozi kuwazuia wananchi waliotaka kuingia kwenye msitu wa jeshi kuutafuta mwili wa mwendesha boda boda huyo maarufu kwa jina la Kaburu aliyepote siku kumi na mbili zilizopita. 

Baada ya kufika kwenye kijiji cha Litapwasi nje kidogo ya mji wa Songea waendesha boda na ndugu wa marehemu waliangua kilio baada ya kuuona mwili wa marehemu Kaburu ukielea kwenye mto Ruvuma na kuliomba Jeshi la polisi kuongeza ulinzi dhidi yao.

Afisa mtendaji wa kata ya litapwasi bw.Dastani luoga amesema kuwa mwili wa mwendesha boda boda huyo uligunduliwa na watoto waliokuwa wakivua samaki kwenye mto ruvuma.
Post a Comment
Powered by Blogger.