Mh Temba atapeliwa shilingi milioni 100

Rapper kutoka TMK Wanaume Family Mh Temba ameelezea sababu za yeye kuwa kimya ni kutokana na kutapeliwa pesa na mfanyakazi wa bandari jijini Dar es Salaam. Temba amekuwa akimposti tapeli wake kupitia ukurasa wake wa Instagram ishara ya kumwinda tapeli huyo na kutangaza donge nono kwa atakayefanikiwa kumpata.

Kupitia kipindi cha Zero Planet ya Ice Fm temba amesema, “Nilishindwa kutoa kazi kwasababu hapa juzi kati nilikua na matatizo sikuweza kuyazunguma sana kwenye media. Kuna jamaa alifanya wizi kakimbia na pesa, ndio maana project zangu hazikuweza kutoka, alinidhulumu pesa nyingi sana.”
Alipoulizwa juu ya kiwango na biashara waliokuwa wanafanya na huyo jamaa, Temba alisema, “tulikuwa tunafanya kazi ya magari, huyo jamaa alikuwa anafanya kazi bandarini alikuwa anadili na haya magari ambayo watu wameshindwa kuyalipia ushuru kwahiyo si tunatoa pesa tunaenda kuyauza, tulikuwa na chama chetu cha washikaji kama 18 hivi kila mtu akatoa pesa kama milioni mia moja na kitu hivi,” ameongeza.
Amesema kumbe hata safari ya South Africa walivyoenda kushoot video ya ‘Waache Waowane’ ya Chege, Temba naye alikwenda kushoot video ya wimbo wake mpya japo hakufanikiwa na majanga yalipoanzia baada ya kuona jamaa hawatumii mkwanja kutoka kwenye biashara zao. Walivyorudi bongo ndio wakajua kuwa jamaa kawapiga mkwanja.
Temba na Chege kwa sasa wanafanya vizuri na wimbo mpya uitwayo ‘Go Down.’

Post a Comment
Powered by Blogger.