MATANGAZO....
pamoja blogBABA

HABARI

MATUKIO

Michezo imedhaminiwa na

MICHEZO

Simulizi zimedhaminiwa na

SIMULIZI

JAMII

BURUDANI

UCHUMI

MAGAZETI

VIDEO ZETU

» » » » Kesi ya Lissu yapigwa kalenda


Pamoja Blog 3/09/2017 03:45:00 PM 0

Kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirishwa hadi Aprili 3, mwaka huu.
Kwa mujibu wa kesi hiyo ambayo ipo katika hatua ya usikilizwaji wa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Godfey Mwambapa imeahirishwa kwa sababu yupo likizo.
Lissu ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) anadaiwa kutoa kauli za uchochezi dhidi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
Anadaiwa kuwa Juni 28, mwaka huu, Lissu akiwa katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, alitoa kauli za uchochezi kuwa:“Mamlaka ya Serikali mbovu ni ya kidiktekta uchwara inahitaji kupingwa na kila Mtanzania kwa nguvu zote, huyu dikitekta uchwara lazima apingwe kila sehemu. Kama uongozi utafanywa na utawala wa kijinga nchi inaingia ndani ya giza nene.’’

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments