Jafo ampa mkandarasi siku 22 kukamilisha ujenzi wa stendi

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Suleiman Jafo ametoa siku 22 kwa mkandarasi anayejenga stendi kuu ya mabasi Korogwe kukamilisha kazi hiyo, kinyume na hapo atakatwa fedha.
Akizungumza baada ya kukagua ujenzi wa stendi hiyo unaoendelea mjini Korogwe , Jafo amesema amelazimika kufanya hivyo baada ya mkandarasi huyo Namis Corporate Ltd ya Dar es Salaam kuongezewa siku 45, lakini bado haonyeshi kumaliza ndani ya siku hizo zinazoishia Machi 30, mwaka huu.
"Mkataba wako umebakiza siku 22 kumalizika. Mimi nasema usije ukapitisha muda huo, hivyo na kupa hadi Machi 30 mwaka huu uwe umemaliza, ukipitisha hapo tunakukata fedha ambazo bado hatujakulipa,”amesema Jafo.
Waziri Jafo ameutaka uongozi wa halmashauri ya Mji Korogwe kusimamia na kuhakikisha ujenzi wa stendi mpya unakamilika kwa wakati.
Post a Comment
Powered by Blogger.