COCA-COLA YAZINDUA MUONEKANO MPYA NA KUAMSHA SHANGWE MKOANI MBEYA LEO

Mkurugenzi Mtendaji wa Coca-Cola Kwanza Bw. Basil Gadzios akionja msisimko na muonekano mpya wa Coca-Cola kwanza Uliobatizwa jina la Amsha Shangwe na Coca-Cola uliozinduliwa leo katika kiwanda cha Coca-Cola kwanza kilichopo maeneo ya Iyunga jirani na Tazara mkoani Mbeya Jijini Mbeya, na hatimaye timu nzima ya Coca-Cola kuzama Mtaani na kutambulisha muonekano Mpya wa Coca-Cola Amsha shangwe kwa wanambeya wote Mkoa na Wilaya zake kuanza kumsha shangwe na Coca-Cola kuanzia hii leo.

Brand Manager wa Coca-ColaTanzania, Sia-Louise Shayo akizungumza jambo mbele ya wafanyakazi na wadau wa Coca-Cola kwanza (hawapo pichani) Katika hafra fupi ya kuzindua kampeni ya muonekano mpya wa Coca -Cola mkoani Mbeya uendao kwa jina la Amsha Shangwe na Coca-Cola kwa wakazi wa Mkoa wa Mbeya.
Marketing Manager wa Coca-Cola Kwanza, Bw. Peter Mpara naye alipata fursa ya kuelezea muonekano huo wa Amsha Shangwe na Coca-Cola kwa wakazi wa Mkoa wa Mbeya Katika hafla fupi ya kuzindua kampeni ya muonekano mpya wa Coca -Cola Mkoani Mbeya uendao kwa jina la Amsha Shangwe na Coca-Cola kwa wakazi wa Mkoa wa Mbeya.
Baadhi ya Wafanyakazi na wadau wa Coca-Cola kwanza wakipata burudani ya muziki sanjari na kupiga picha kwa pamoja kwa kuamsha shangwe na Coca-ColaKatika hafra fupi ya kuzinduwa kampeni ya muonekano mpya wa Coca -Cola Mkoani Mbeya uendao kwa jina la Amsha Shangwe na Coca-Cola kwa wakazi wa Mkoa wa Mbeya.
Post a Comment
Powered by Blogger.