Bilionea David Rockefeller Mmarekani afariki akiwa usingizini

Alikuwa na umri wa miaka 101.
Bilionea Mmarekani anayefahamika pia kwa kutoa pesa za hisani kuwasaidia wasiojiweza David Rockefeller amefariki dunia akiwa usingizini nyumbani kwake Poncantico Hills, New York.
Bw Rockefeller alikuwa mtoto wa mwisho kwenye familia hiyo maarufu nchini Marekani.
Alikuwa mjukuu wa mwanzilishi wa kampuni ya Standard Oil John D Rockefeller.

Mzee huyo ndiye aliyekuwa anasimamia mali na biashara za familia hiyo, pamoja na miradi yake ya kusaidia jamii.
Watu wanane matajiri kupindukia duniani.

Ingawa hakuwahi kutafuta wadhifa wowote wa kisiasa, kaka zake wawili walihudumu serikali.
Post a Comment
Powered by Blogger.