WAZIRI MWIJAGE KUFUNGUA MSIMU MPYA WA MAFUNZO YA WASICHANA YANAYODHAMINIWA NA TAASISI YA MANJANO

Mwasisi wa Taasisi ya Manjano na Mmiliki wa Shear Illusions, Shekha Nasser akizungumza na waandishi wa habari leo kuanza kwa msimu mpya wa mafunzo ya wajasilimali wasichana kwa mikoa mbalimbali hapa nchini.
Lucy John kutokea Temeke  akizungumza namna alivyochaguliwa na kujiunga kwenye mafunzo ya ujasialiamali kutoka Taasisi ya Manjano.
Baadhi ya wasichana waliochaguliwa kwenye mafunzo ya ujasiliamali wakiwa kwenye mkutano wa waandishi wa habari

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Waziri wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage anataraji kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi ya mafunzo ya wajasiliamli wasichana jijini Dar es Salaam leo yanayodhaminiwa na Taasisi ya Manjano.

Shear Illusion kupitia Taasisi ya Manjano imeanzisha mpango maalum wa kusaidia kutoa ajira kwa wanawake ambao wamemaliza shule na kushindwa kupata kazi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo afisa mtendaji mkuu wa Shear Illusions Ltd Shekha Nasser amesema ameamua kumualika mwijage hili aweze kuona fursa zilizopo katika viwanda vidogo.

Amesema kuwa mara baada ya kuona tatizo hilo wakaamua kuanzisha mradi wa uuzaji wa bidhaa za manjano kwa wanawake mbalimbali waliopo jijini Dar es Salaam na mikoa mingine.

“Tasnia hii ya urembo ni moja ya vitu vinavyoweza kumsaidia mwanamke kuingiza zaidi ya shilingi milioni mbili kwa mwezi kama mtu atakuwa mwaminifu na biashara kuifanya hii kuwa ni kazi yake ya muhimu katika kujikwamua kiuchumi” amesema. Shekha Nasser

Amesema kuwa katika kuhakikisha kuwa wanatoa ajira kwa wasichana hao wameamua kutoa mafunzo ya wiki mbili kwa wasichana 30 ambao watapewa mtaji wa shilingi 300,000/-

Amesema kuwa wasichana hao ambao wapo 30 wamepatikana kutokana na mchujo uliofanywa na watalaamu wa masuala ya urembo hadi kufikia hapo .
Post a Comment
Powered by Blogger.