WAKUU WA SHULE NA WAKURUGENZI DAR WATAKIWA KUTOA SABABU ZA SHULE ZAO KUFELI

Kufuatia Dar es Salaam kufanya vibaya katika mtihani wa kidato cha nne kwa mwaka 2016 kwa kuingiza shule 6 kati ya kumi zilizofanya vibaya, ofisi ya Elimu Mkoa imewaagiza wakuu wa shule na wakurugenzi kutoa taarifa za kina juu ya sababu zilizopelekea kufanya vibaya.

Akiongea na TBC, kaimu Afisa elimu mkoa, Janeth Nsunza, alisema bado wanaendelea na kikao kujadili tathmini ya matokeo hayo na wamesema watatoa taarifa kamili watakapomaliza majadiliano.
Alisema, “Kati ya shule 10 ambazo hazikufanya vizuri shule hizo ni Kitonga, Nyeburu, Mbopo, Mbondole, Somangila day na Kidete kufuatia shule hizo sita kutofanya vizuri mkoa wa Dar es Salaam, mkoa umepokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa kwani imekuwa ni kinyume cha matarajio yetu na serikali yetu kwa ujumla.”
“Kwakuwa matokeo yametanganzwA, hatua za kufahamu nini hali hiyo imejitokeza zimechukuliwa mara baada ya matokeo hayo kutangazwa ambapo wahusika wanaendelea kutoa maelezo yao, licha kwa kuwepo kwa viashiria katika mtihani wa Mock na wakurugenzi waliwaelekeza wakuu wa shule hizo kuondoa hali hizo mapema,” aliongeza Nsunza.

Post a Comment
Powered by Blogger.