Wachimbaji wengine wafukiwa na kifusi Mara

Takriban mwezi mmoja tangu wachimbaji 15 wafukiwe na kifusi Nyarugusu wilayani Geita, balaa jingine la aina hiyo limetokea wilayani Butiama mkoani Mara.

Katika tukio la Butiama, watu 11 wameokolewa shimoni wakichimba dhahabu na kwa sasa wamelazwa Hospitali ya Wilaya ya Butiama kwa matibabu.
Mkasa huo umetokea katika Mgodi wa Buhemba na Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi amesema kazi ya uokoaji inaendelea kwa ajili ya kuwatafuta watu wengine ambao ndugu zao hawajawaona na wanahisi walikuwamo ndani ya shimo hilo.
Amesema mmomonyoko wa udongo ndiyo uliosababisha kuporomoka kwa mashimo hayo ya muda mrefu licha ya kuwapo jua kali.
Aidha Nyamubi amesema mashimo hayo yaliyoachwa na mkoloni yako chini ya mwekezaji StanCom ambaye ndiye aliyekuwa akichimba dhahabu katika eneo hilo. Kufuatia tukio hilo, viongozi mbalimbali walifika kushuhudia uokoaji akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Mara, Dk Charles Mlingwa.

Chanzo: Mwananchi
Post a Comment
Powered by Blogger.