VIDEO: MAKONDA AWAANIKA WANAOTUMIA NA KUFANYA BIASHARA HIYO, WAKO WASANII NA ASKARI 9

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataja askari 9 wanaotuhumiwa kushirikiana na wafanya biashara ya madawa ya kulevya.
Aidha amewataja wasanii wanaojihusisha na matumizi na uuzaji wa Madawa ya kulevya na kuwataka kuripoti kituo cha polisi kesho.
Akiongea na waandishi wa habari akiwa ofisini kwake Alhamisi hii, RC Makonda amewataka wauzaji wote kufika makao makuu ya polisi kwajili ya kujieleza.

“Nimeamua kuingia kwenye hii vita kwa sababu najua siku moja Mungu ataniuliza, nilikupa mkoa wa Dar es salaam kupitia Rais John Pombe Magufuli watoto waliangamia kwa Madawa ya kulevya, sitaki kufika mbungini nisiwe na jibu, nipo tayari kupoteza ukuu wangu wa mkoa, nipo tayari kutangulia kwa aliyeniumba lakini niwe na jibu kwa mungu wangu aliyeniumba kwamba Madawa ya kulevya hayakubaliki ndani ya Dar es salaam,” alisema Makonda.
Aliongeza,’Wapo tuliowakamata pamoja na dawa zao tumeshawafikisha Central Polisi na wanaendelea na mambo yanayotakiwa. Lakini wapo ambao bado, majina ni mengi sana mtayapitia wenyewe, kuna Mchafu, Director Joan, Mirror, Rommy na wengine wengi, wapo wauzaji wadogo na wengine wakubwa. Lakini wapo wengine wanasemekana wanatumia lakini hakuna ushahidi kwamba wanatumia ingiwa wenzao wanasema wanatumia, ni bora nikakutana nao kesho pale Central, akiwemo TID, Wema Sepetu,”


List ya watuhumiwa

RC Makonda amewataja wanaotuhumiwa kutumiwa dawa za kulevya wakiwemo TID, Wema Sepetu, Chid Benz, Recho, amewataka kesho wakutane polisi

Kuna maeneo watu wanatuambia madawa ya kulevya wanayapata sehemu hizo, wamiliki wake kesho niwakute polisi, wasipokuja nitawafuata - RC Makonda

Kama unajua una eneo unafanya biashara za dawa za kulevya DSM natoa siku 7 biashara hii iishe, operesheni hii naiongoza mwenyewe - RC Makonda

Kama Kamishna Sirro na timu yake watashindwa kutokomeza dawa za kulevya DSM maana yake wamekosa sifa za kuendelea kuwa askari - RC Makonda

Watano tayari nimeshawakamata na wengine nimewakamata wakiwa na dawa za kulevya - RC Makonda


Post a Comment
Powered by Blogger.