UPDATES: MASOGANGE AFIKISHWA KISUTU, APEWA DHAMANA

Mrembo anayepamba video za wanamuziki, Agness Gerald, maarufu kwa jina la Masogange na wafanyakazi 14 wa kampuni ya Quality Group wamefikishwa katika Mahakama ya Kisutu wakisubiri kusomewa mashitaka.
Masogange ambaye alikamatwa wiki iliyopita kwa tuhuma za kujihusisha na madawa ya kulevya amefikishwa mahakamani hapo leo Jumatano asubuhi akiambatana na wafanyakazi wa Quality Group.
Wafanyakazi hao wa Quality Group wanadaiwa kufanya kazi nchini bila kuwa na vibali baada ya kukamatwa na Ofisa Uhamiaji wa Mkoa wa Dar es Salaam, John Msumule.
Post a Comment
Powered by Blogger.