UPDATES: IDD AZZAN AWASILI KITUO CHA POLISI CHA KATI KWA AJILI YA MAHOJIANO

Mbunge wa zamani wa Kinondoni, Iddy Azzan ameripoti katika kituo cha polisi cha kati kama aliyotakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Azzan amewasili kituoni hapo muda wa saa 09:06 kwaajili ya mahojiano na polisi baada ya kutakiwa kufanya hivyo na mkuu wa mkoa.
Azzan ni miongoni mwa watu 65 waliotajwa na mkuu wa mkoa juzi kutakiwa kufika polisi jijini Dar es Salaam.
Jana Askofu wa kanisa la ufufuo uzima Josephat Gwajima na mfanyabiashara maarufu, Yusuf Manji ambao nao wapo katika orodha hiyo ya mkuu wa mkoa waliripoti.
Kamanda wa Kanda Maalumu, Simon Sirro amesema ifikikapo saa 7 mchana atazungumza na waandishi wa habari.
Post a Comment
Powered by Blogger.