TGNP MTANDAO WAADHIMISHA SIKU YA UKEKETAJI KWENYE KATA YA KUPUNGUNI JIJINI DAR

 Mratibu wa programu ya harakati na nguvu ya pamoja kutoka TGNP Anna Sangai akizungumza leo wakati wa maadhimisho ya kitaifa ya siku ya ukeketaji duniani kwa njia ya majadiliano yaliyofanyika katika mtaa wa Kipunguni B.

Uwepo wa watu jamii ya wakurya kwa asilimia 75% umesababisha Kata ya Kipunguni iliyipo manispaa ya Ilala mkoa hapa kuongoza kwa vitendo vya ukeketaji wa wanawake ndani ya mkoa.

Haya yalibainishwa leo wakati wa maadhimisho ya kitaifa ya siku ya ukeketaji duniani kwa njia ya majadiliano yaliyofanyika katika mtaa wa Kipunguni B katani humo ambapo mratibu wa programu ya harakati na nguvu ya pamoja kutoka TGNP Anna Sangai alisema  mapambano ya vitendo hivyo yanakwamishwa na utashi wa watu kutoa taarifa.

"Kata ya kipunguni ina jumla ya wakazi 36,000 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, Asilimia 75 ya wakazi hao ni wenyeji wa Mkoa wa Mara ambao ndiyo wanaoendekeza mfumo huo wa ukeketaji kama ilivyo katika mkoa wao ambao unyanyasaji huo wa kijinsia upo kwa asilimia 40%," anasema Sangai.

Mbali na changamoto ya utoaji wa taarifa Sangai alisema tatizo lingine ni mfumo dume na ukosefu wa rasilimali kwakuwa mangariba wanaoendekeza vitendo hivyo ni kwaajili ya kujipatia fedha kwani hupata Sh 20,000 baada ya kumkeketa mschana mmoja.

Aliongeza kuwa ukeketaji umekuwa ukiendea kushamili licha ya hatua zinazochukuliwa Kwani awali vitendo hivyo vilikuwa vinafanyika vijini lakini sasa hata mjini " Sasa wakeketaji wanebuni njia mpya mtoto hukeketwa mara baada ya kuzaliwa na kama ni mkubwa anavarishwa nguo za kiume ili watu wasiweze kujua pindi anapokuwa anapelekwa jando".

Kwa upande wake Daniel Maragashimba akizungumza kwa niaba ya Diwani wa kata hiyo alisema kwa asilimia kubwa kata hiyo imeathiriwa na vitendo hivyo ambavyo ni matokeo ya wakurya kuanzisha utamaduni wao katika eneo hilo,  lakini hata hivyo wakazi wake wamekuwa ni wagumu kutoa polisi katika madawati ya jinsia na jeshi la polisi.

"Kinachotakiwa sasa sio kutoa elimu kwa wazazi tena kama ilivyozoeleka bali bali elimu ya jamii nzima wakiwemo watoto kama inavyofanyika katika mapambano ya ukati mwingine wa kijinsia," alisema Maragashimba.

Mkazi wa Kipuguni Tausi Msangi alisema wananchi wamekuwa wakimbana na vitendo hivyo "Kuanzia mwaka 2015 hadi leo tulifanikiwa kuzuia ukeketaji wa watoto 150, Mangariba wawili wameacha kukeketa baada ya kupatiwa elimu na Ngariba mmoja amefikishwa mahakamani na kesi yake inaendelea".
 Daniel Maragashimba akizungumza kwa niaba ya Diwani wa kata kuhusu mchango wa Kata hiyo katika utetea haki za wanawake pamoja na kupinga unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto wa kike.
Mwanaharakati wa Sauti ya Jamii Kipunguni, Fatma Abdulhamani akizungumza na waaanaharakati wa kata hiyo wakati wa maadhimisho ya kitaifa ya siku ya ukeketaji duniani

 Mkazi wa Kipuguni Tausi Msangi akisoma mafanikio pamoja na changamoto wanazozipata katika utoaji wa elimu hasa kwa watoto wadaogo ambao bado hawajakeketwa 
Mjumbe wa Nyumba 10 Kata ya Kipunguni, Hija S. Mzome akizungumza kuhusu ukeketaji kuwa umekuwa ukiendea kushamili licha ya hatua zinazochukuliwa Kwani awali vitendo hivyo vilikuwa vinafanyika vijini lakini sasa hata mjini 
Baadhi ya wadau wa kupigania haki za wanawake wakichangia mada
Post a Comment
Powered by Blogger.