SUMU YA PENZI SEHEMU YA THEMANINI NA MBILI (82)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Nilikuja kushtukia nipo hospitali na nilishonwa nyuzi tano. Daktari aliniambia nilikuwa na bahati jeraha lilikuwa juu ya jicho na laiti kama Hadija angenilenga jichoni basi ningekuwa chongo.
Mh! japo nilikuwa kiburi kwenye suala la kumuomba Mungu, aisee siku hiyo nilijikuta nikimshukuru Mungu mno maana Hadija alionekana wazi kabisa kukusudia kuharibu uso wangu. Nadhani alifahamu fika kuwa pengine sura yangu ikiwa na hitilafu ndiyo mapenzi ya mume wangu yatapungua.
Nikakumbuka habari ambazo mara kwa mara huwa nazisikia kuwa mwanamke kachanwa usoni na viwembe au kamwagiwa maji ya moto; yote hayo yanatokana na kuwa wanaringia uzuri wao kwenye mapenzi, kwa hiyo wengine wanadhani hiyo ndiyo dawa ya kuwakomesha.
Na ni kweli kabisa, sasa fikiria kama mpenzi wako anakupenda kwa jinsi ulivyo na sura ya kuvutia, siku ukiungua, au umekuwa chongo kama nilivyonusurika mimi, unafikiri kutakuwa na mapenzi tena hapo!
Kuna mchekeshaji mmoja maarufu wa Uingereza karne ya 20, alikuwa akiitwa Charlie Chaplin huyu jamaa alishawahi kuandika kuwa ‘Your Naked Body Should Belong to someone who is in love with your Naked Soul.” Akiwa na maana; “utupu wa mwili wako apewe mtu ambaye ana mapenzi ya dhati na utupu wa roho yako.”


UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO AU ZILIZOPITA ZILIZOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 NA KAMA HUNA WHATSAPP PIGA SIMU UPEWE MAELEKEZO YA   KUTUMIWA

ITAENDELEA JUMAMOSI

Post a Comment
Powered by Blogger.