SUMU YA PENZI SEHEMU YA THEMANINI NA TANO (85)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


“hii baa ina matatizo gani? Tumekuja hapa dakika nzima hakuna wahudumu wala nini au tuondoke!” nilimfokea huyo mwanaume bila kujali mguu wa Gululi aliyekuwa akinigonga kwa chini.
“hapana dada msiondoke popote niombe radhi,” alisema na kuita mhudumu mmoja kwa amri. Akaanza kuwakoromea wale wahudumu e na kuwataka watusikilize haraka sana.
Basi mhudumu mmoja akaja na alipochukua oda na kuondoka, nikamuuliza sasa vizuri Gululi.
“ndiyo huyu!”
“ndiyo yeye.”
“anafanya nini mbona amekuja kibosibosi?”
“mh nilisikiaga ni meneja wa baa, inawezekana!” Alisema Gululi.
“sikia nimeona anavyokutolea macho, sasa hiyo ni hatua nzuri lakini usije ukajilegeza kwa chochote.. la sivyo atakutumia na kukuacha tena..” nilimuonya Gululi tena nikimtaka hata asimuangalie.
Nilipochunguza vizuri nikagundua  kumbe ile baa ina upande wa lodge hapohapo. 
Tena nikamuangalia mume wa Gululi nikagundua ni wakujakuja  yaani alionekana amechelewa kujanjaruka kwa hiyo hakuwa na tatizo la kurudishwa kwenye mstari.
Yaani anaweza kuwa amechepuka na kumuacha mkewe kwa ajili tu ya fasheni au kufuata mkumbo wa marafiki, wanaume kama hao wapo, unakuta kisa marafiki zake wana wasichana wa aina fulani na yeye unakuta anamdharau mkewe au mpenzi wake wa muda mrefu ili kuwa na msichana wa aina hiyo ili mradi tu apate sifa kwa hao marafiki zake.


UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO AU ZILIZOPITA ZILIZOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 NA KAMA HUNA WHATSAPP PIGA SIMU UPEWE MAELEKEZO YA   KUTUMIWA

ITAENDELEA JUMANNE
Post a Comment
Powered by Blogger.