SUMU YA PENZI SEHEMU YA THEMANINI NA TATU (83)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Huwezi amini sasa nyumba ilitulia, ikabidi ratiba yetu ya sherehe ya utambulisho ihuishwe kama kawaida, tukawa tunasubiriwa sisi tu tupone kwanza vile vijeraha vyetu ili tusije tukachekesha kwenye harusi.
Basi wiki moja kila kitu kilikuwa tayari, huwezi amini kile kijeraha pembeni ya jicho hakikuniharibu hata kidogo, sanasana kikaniongezea urembo wangu na hata Mr X wangu naye alikuwa hivyohivyo.
“baba we are ready! (tupo tayari),” nilimwambia baba nikiashiria kwamba hata kesho au kesho kutwa tufanye sherehe yetu ya utambulisho maana niliisubiria kwa hamu sana. “hivi nyinyi hayo makovu mliambiazana muumie pamoja au?” aliuliza baba kiutani na kucheka.
Haikupita siku nyingi sana, ndugu marafiki, watu wa karibu wote walitaarifiwa na sherehe ya utambulisho tulipanga ifanyike Mlimani City, na mimi nikahakikisha nawatumia kadi ya Mwaliko Kungwi wangu Bibi Gululi na mwanaye Gululi, pia nikawatumia kadi rafiki zangu Getrude na Catherine.
Hayawihayawi sasa yamekuwa; siku ikafikia, ndugu zangu kibao kutoka mikoani na hapa mjini wakajaa na kujazana, na wengine hata ambao sikuwa nikiwafahamu, wengi wakawa wanakuja na kunipongeza kwa kuolewa na mtu wa mamtoni.

UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO AU ZILIZOPITA ZILIZOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 NA KAMA HUNA WHATSAPP PIGA SIMU UPEWE MAELEKEZO YA   KUTUMIWA

ITAENDELEA JUMAPILI
Post a Comment
Powered by Blogger.