SUMU YA PENZI SEHEMU YA SABINI NA TANO (75)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Wakati anasema hayo haraka Yule mwanasheria akatoa kopi ya ule ujumbe wa baba na kututaka twende polisi kwa msaada wa haraka. Kweli tukatoka pale na kuelekea polisi kituo cha Mbezi kwa Yusufu. Baada ya mimi kuwaelezea hali ilivyo nikapelekwa kuonana na mkuu wa kituo.
Nashukuru Mungu hakukuwa na magumashi, nikafungua jalada na kupewa polisi kuelekea nao kwa akina Fatuma.
Kama kawaida pale nje kwao tulimuona bibi yake akiwa amekaa kwenye mkeka, alivyoniona akashtuka.
“bibi sisi ni maofisa polisi kutoka kituo cha Mbezi kwa Yusufu, tumekuja kumuulizia mjukuu wako Fatuma yupo?” aliuliza afande mmoja.
“Hayupo! Kwani kafanya nini?”
“anashukiwa kutaka kufanya jaribio la mauaji kwa mzee Geofrey, kuna ushahidi kutoka kwa hawa  wanaye.” Alisema Yule afande.
“Mauaji? Huyo mzee Geofrey si ni mume halali wa mjukuu wangu, na wameoana jana hapa nyumbani.” Alisema Yule bibi. Nikamtazama Mage nikamuona anachungulia kitu kupitia ubavu wa ile nyumba.
“bibi kama Fatuma hayupo! Ndani kuna nani?” aliuliza Mage.
“ndani hakuna mtu yoyote..”

UKITAKA KUSOMA STORY YA LEO AU ZILIZOPITA ZILIZOKAMILIKA NITAFUTE WHATSAPP KWA NAMBA HII 0713363965 NA KAMA HUNA WHATSAPP PIGA SIMU UPEWE MAELEKEZO YA   KUTUMIWA


ITAENDELEA JUMAMOSI
Post a Comment
Powered by Blogger.